1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo vya ajali mbaya ya barabarani Kenya yafikia 49

1 Julai 2023

Idadi ya vifo kutokana na ajali mbaya kabisa ya barabarani Magharibi mwa Kenya imepanda hadi watu 49. Waokoaji walikuwa na wakati mgumu kuyaondoa mabaki ambapo waathiriwa zaidi walihofiwa kunaswa.

Kenia Tote bei schwerem Autounfall
Picha: AP/dpa/picture alliance

Polisi ilisema lori ilipoteza mwelekeo na kuyaparamia magari kadhaa na watu katika makutano ya barabara yenye shughuli nyingi jana jioni. Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amewaambia waandishi habari katika eneo la mkasa huo la LONDIANI kuwa idadi ya vifo sasa ni 49.

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara kuu kati ya mji wa Nakuru na Kericho. Mkuu wa Mkoa wa Bonde la Ufa Abdi Hassan amesema zaidi ya watu 30 pia walijeruhiwa wakati lori hiyo ilipoyagonga magari madogo, bodaboda na vibanda vya wauzaji.

Hatima ya dereva wa lori hiyo haijajulikana. Viongozi wa Kenya akiwemo Rais William Ruto walituma salamu za rambirambi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW