1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo vya mafuriko ya Libya yafikia 3,753

23 Septemba 2023

Idadi ya vifo vilivyothibitishwa kutokana na mafuriko makubwa ambayo yamelikumba eneo la mashariki mwa Libya takribani wiki mbili zilizopita, imeongezeka na kufikia watu 3,753

Libyen Darna Mann sitzt in den Trümmern
Picha: KARIM SAHIB/AFP

Akizungumza na waandishi wa habari hivi leo, afisa kutoka katika kamati ya kukabiliana na dharura kwa upande wa serikali ya mashariki, Mohamed Eljarh, amesema idadi hiyo ya vifo inajumuisha miili 168 iliyogundulika Alhamis.Tangu kutokea kwa maafa hayo Septemba 10 mwaka huu, kumekuwa na takwimu zinazotofautiana kuhusu idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko kwa taifa hilo lililogawanyika kisiasa.Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watu 4,014 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 8,500 hawajulikani waliko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW