1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uvamizi wa Israel wasababisha vifo Ukingo wa Magharibi

31 Agosti 2024

Idadi ya waliouawa kufuatia operesheni ya siku tatu ya Israel kwenye Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu imeongezeka hadi kufikia watu 20.

Wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye operesheni katika Ukingo wa Magharibi
Wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye operesheni katika Ukingo wa MagharibiPicha: Majdi Mohammed/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na mamlaka za Israel pamoja na Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina. Israel imedai kuwa mashambulizi hayo yanayolenga miji na kambi za wakimbizi kote kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi kuwa ni ya kupambana na ugaidi.

Soma pia: Israel yaendeleza operesheni Ukingo wa Magharibi

Hayo yanaripotiwa wakati mapigano yakiendelea pia katika Ukanda wa Gaza. Medo Halimi, kijana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 19 aliyejizolea umaarufu kwenye mtandao wa TikTok kwa kuonyesha maisha ya Gaza wakati wa vita, ameuawa kwa shambulio la Israel.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW