1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMorocco

Idadi ya vifo yaongezeka Morocco na kukaribia watu 2,900

12 Septemba 2023

Idadi ya vifo kufuatia tetemeko la ardhi nchini Morocco imefikia karibu watu 2,900 huku wengine zaidi ya 2,500 wakiwa wamejeruhiwa. Vikosi vya uokoaji vimeendelea bila kuchoka kuwatafuta manusura usiku kucha.

Erdbeben in Marokko - Einsatzkräfte bei Aufräumarbeiten
Zoezi la uokoaji likiendelea katika mji wa Marrakesh, MoroccoPicha: Said Echarif/AA/picture alliance

Vikosi vya uokoaji vimeendelea bila kuchoka kuwatafuta manusura usiku kucha.

Morocco imekuwa ikikosolewa kuchelewesha kutoa idhini kwa mashirika mengine ya uokoaji kuingia nchini humo ili kutoa msaada.

Maafisa wa Morocco wanasema uamuzi huo unalenga kuepuka mkanganyiko katika uratibu ambao wanadai hautokuwa na manufaa yoyote.

Soma pia:Tetemeko la ardhi Morocco: Idadi ya vifo yakaribia 2,900

Ufaransa imetangaza msaada wa dharura kwa Morocco wa dola milioni 5.4 utakaolekezwa kwa mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yanayoendelea kutoa msaada nchini humo.

Hili ni tukio baya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyoya Kaskazini mwa Afrika tangu tetemeko la ardhi la mwaka 1960 lililoharibu mji wa Agadir na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.    

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW