DRC: Maambukizi ya Ebola yaongezeka, wahudumu wa afya wagoma
9 Julai 2026
Matangazo
Hayo yanaarifiwa wakati wahudumu wa afya katika maeneo yaliyoathirika zaidi na mlipuko huo wa Ebola nchini Kongo, wamegoma kufanya kazi wakisema hawajalipwa mishahara yao tangu Mei 15 huku wakifanya kazi katika mazingira duni.
Stephen Mapesa, naibu mkuu wa mfumo wa afya katika jimbo la Ituri, kitovu cha mlipuko huo amesema wahudumu wa afya katika miji kadhaa iliyoathiriwa mno na Ebola, wamejiunga na mgomo huo, wakidai malipo ya juu na mazingira bora ya kazi.
Mgomo wa kitaifa wa wahudumu wa afya unaohofiwa , unaweza kutatiza juhudi za kudhibiti ugonjwa huo unaoendelea kuenea kwa kasi zaidi huku hatua za kukabiliana nao zikisuasua.