1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya visa vya ebola yaongezeka Kongo

Josephat Charo
11 Juni 2026

Idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka hadi 635. Misri imeahidi kuisaidia Kongo katika suala la ebola.

Wafanyakazi wa afya wa Kongo wakiwa wamevaa vifaa vya kujikinga (PPE) wakiwabeba watoto waliopimwa na kuondolewa Ebola kutoka kituo cha watoto yatima cha Saint Nicholas, katika Kituo cha Evangelique cha Matibabu (CME) huku mashirika ya misaada yakiongeza juhudi za kudhibiti mlipuko wa Ebola wilaya ya Hoho ya mji wa Bunia, mkoa wa Ituri Juni 9, 2026.
Wafanyakazi wa afya wa Kongo wakiwa wamevaa vifaa vya kujikinga (PPE) wakiwabeba watoto waliopimwa na kuondolewa Ebola kutoka kituo cha watoto yatima cha Saint Nicholas, katika Kituo cha Evangelique cha Matibabu (CME) huku mashirika ya misaada yakiongeza juhudi za kudhibiti mlipuko wa Ebola wilaya ya Hoho ya mji wa Bunia, mkoa wa Ituri Juni 9, 2026.Picha: Gradel Muyisa Mumbere/REUTERS

Idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongezeka hadi 635, ikiwa ni pamoja na vifo 127. Idadi hiyo imebainika kwenye data za serikali Jumatano. 

Wakati huo huo, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitangaza ufadhili wa ziada wa dola milioni 20 jana kama sehemu ya kukabiliana na mlipuko wa Ebola barani Afrika.

Wakati haya yakiarifiwa, rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi Jumatano alisisitiza kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa ziara ya rais wa Kongo, Felix Tshisekedi huko Cairo.

El-Sissi alisema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kufuatia mazungumzo akielezea mshikamano wa Misri na Kongo katika kukabiliana na mgogoro wa sasa wa kibinadamu katika sehemu ya mashariki ya nchi na utayari wao wa kutoa aina zote muhimu za msaada wa kimatibabu, chakula na misaada ya kibinadamu katika suala la ebola.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW