1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wagonjwa wa homa ya mafua yaongezeka Uingereza

9 Januari 2025

Maafisa wa afya nchini Uingereza wamesema idadi ya watu waliolazwa hospitali kutokana na homa ya mafua nchini humo inaendelea kuongezeka.

Takwimu kutoka huduma ya kitaifa ya afya nchini humo NHS zinaonyesha kwamba, kulikuwepo wastani wa wagonjwa 5,408 wa homa ya mafua waliolazwa hospitali kila siku wiki iliyopita, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 256 waliokuwa kwenye huduma za dharura.

Takwimu hii ni ongezeko la asilimia 21 kutoka wagonjwa 4,469 wiki iliyopita ambapo wagonjwa 211 walihitaji huduma za dharura.

Pia idadi hiyo ni karibu mara tano ya idadi ya wagonjwa waliolazwa mnamo Desemba mosi, wakati huo kulikuwepo wagonjwa 1,098.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW