Idadi ya waliofariki kwa moto wa nyika Marekani yafikia 24
13 Januari 2025Mamlaka katika eneo hilo zimeonya kuwa moto mpya unaweza kuzuka kutokana na upepo mkali. Anthony Marrone ni Mkuu wa Idara ya zimamoto mjini Los Angeles.
"Maelfu kwa maelfu ya vitu vinavyowaka, tena mapande makubwa makubwa yanapeperushwa na upepo na hii inaweza kusambaza moto zaidi."
Soma pia:Wazima moto wapambana kuzuia moto Los Angeles katikati ya tahadhari ya upepo mkali
Huduma ya kitaifa ya hali ya hewa imetoa onyo juu ya moto mkali zaidi kuanzia kesho siku ya Jumanne na Jumatano. Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani ya White House ni kwamba watu 24,000 wamejiandikisha ili kupatiwa msaada kufuatia maafa hayo.
Moto huo umeteketeza makazi ya watu na kuuharibu kabisa mji wa Los Angeles uliopo katika jimbo la California na kuwaacha maelfu bila makazi.