1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliokufa kufuatia maporomoko ya ardhi Ethiopia yafikia 157

23 Julai 2024

Idadi ya vifo vilivyotokana na matukio mawili ya maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia vimeongezeka kwa kasi hadi 157 na serikali ikisema idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi.

Ethiopia
Waliokufa kufuatia maporomoko ya ardhi Ethiopia yafikia 157Picha: Gofa Zone Government Communication Affairs Department

Idadi ya vifo vilivyotokana na matukio mawili ya maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia vimeongezeka kwa kasi hadi 157 na serikali ikisema idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi.

Taarifa ya serikali inasema maporomoko ya ardhi yamefukia watu katika eneo la Gofa Kusini mwa Ethiopia, na  katika pirika za uokozi lilitokea lingine katika eneo hilohilo na kuwakumba walokuwa wakitoa msaada.

Mkuu wa Wakala wa Kitaifa wa Kukabiliana na Maafa katika Kanda ya Gofa, Markos Melese, amesema kazi ya kutafuta manusura na miili ya waiokufa bado inaendelea. Na kuongeza kuwa eneo hilo lina changamoto nyingi sana.

Taarifa rasmi kutoka katika eneo hilo alisema takribani watu 50 wamekufa na kwamba watoto na maafisa wa polisi ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW