1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa kwa mkanyagano Nigeria yafikia 32

22 Desemba 2024

Polisi ya Nigeria imesema idadi ya waliofariki kutokana na mkanyagano nje ya vituo vya kusambaza chakula kwa watu maskini imefikia 32.Tukio hilo linajiri wakati nchi hiyo ikikabiliwa na misururu wa matukio kama hayo.

Nigeria
Hali katika eneo la Ibadan nchini Nigeria baada ya kutokea kwa mkanyagano uliogharimu maisha ya watuPicha: Oluwasegun Falomo/Anadolu/picture alliance

Polisi ya Nigeria imesema idadi ya waliofariki kutokana na mkanyagano nje ya vituo vya kusambaza chakula kwa watu  maskini imefikia 32.Tukio hilo linajiri wakati nchi hiyo ikikabiliwa na misururu wa matukio kama hayo kwenye hafla za kutoa misaada.

Hapo jana,  ripoti za polisi zilisema kwamba watu 22 ndio waliopoteza maisha katika mkasa huo uliotokea wakiwa kwenye foleni nje ya kituo cha kusambaza mchele katika mji wa kusini wa Okija na kuonya kwamba idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

Soma zaidi.Frank-Walter Steinmeier aendelea na ziara yake Afrika

Tukio hilo la Jumamosi linafanana na tukio lingine la mkanyagano katika maonyesho ya shule katika mji wa kusini magharibi wa Ibadan siku ya Alhamisi ambapo watoto 35 walipoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametuma salamu za rambirambi kwa wahanga wa mkasa huo. Taarifa kutoka kwa msemaji wa rais Tinubu imeongeza kuwa rais huyo amesitisha shughuli zake rasmi mjini Lagos leo ili kutoa heshima ya wahanga wa mkanyagano huo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW