1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Idadi ya waliokufa nchini Iraq kwenye shambulizi yafikia 32

Saleh Mwanamilongo
21 Januari 2021

Washambuliaji wawili wa kujitoa muhanga wamewauwa watu zaidi ya 32 na kujeruhi wengine wasiopungua 70 mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Irak Selbstmordanschlag in Bagdad
Picha: Thaier al-Sudani/REUTERS

Washambuliaji wawili wa kujitoa muhanga wamewauwa watu zaidi ya 32 na kujeruhi wengine wasiopungua 70 kwenye shambulizi lililotokea leo katikati ya mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Viongozi wamewatuhumu wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu kuhusika na mashambulizi hayo. 

 Jeshi la Iraq limesema watu wawili wenye mikanda ya mabomu wamejilipua ndani ya soko lenye msongamano mkubwa katikati ya mtaa wenye shughuli nyingi mjini Baghdad.

 Maafisa wa polisi na wahudumu wa hospitali wamesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa sababu wale waliojeruhiwa wapo kwenye hali mahututi.

''Namna na adui viko wazi kabisaa''

Meja-Jenerali Kadhim Salman,mkuu wa kikosi cha ulinzi wa kiraia amewambia wandishi habari kwamba huenda wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu ndio waliotekeleza mauwaji hayo.

 Salman alisema kwenye eneo la tukio kwamba idadi ya vifo imefikia 28 kutoka 23 kama ilivyoripotiwa awali na watu wengine 73 walijeruhiwa.

'' Namna na adui viko wazi kabisaa kulingana na ninvyojua, hivyo hakuna tangazo rasmi, lakini kwa uhakika, pengine shirika la kigaidi, la Dola la Kiislamu linahusika na tukio hili la kihalifu.''

Duru za polisi zinaeleza kwamba vikosi vya usalama vimetawanywa na barabara kufungwa ilikuepusha mashambilizi zaidi.Wapiga picha wa shirika la habari la Reuters wameshuhudia madimbwi ya damu muda mfupi baada ya mashambulizi hayo.

Shahidi mmoja amesema kwamba mshambuliaji alikaa katikati mwa watu na kujifanya mgonjwa na baadae akajiripuwa.Ukanda wa video uliosambazwa mitandaoni umeonyesha mripuko wa pili ukiwatawanya watu waliokuwa kwenye eneo hilo. Picha hizo zinaonyesha watu wengi ambao wameonekana wamekufa au wamejeruhiwa.

Uchaguzi wa mapema waitishwa Oktoba

Picha: picture alliance/dpa/Planet Pix/Zuma/Lt. Col. A. Weale

Wizara ya afya ya Irak, ilitangaza kwamba hospitali zote zilihamasishwa ili kuwahudumiwa watu waliojeruhiwa.

Jenerali Tahsin al-Khafaji, msemaji wa operesheni ya vikosi vya pamoja vya Irak, ameyaita mashambulizi hayo kuwa kitendo cha ugaidi kilicho fanywa na kundi lisilo jitambulisha la Dola la Kiislamu ambalo linataka kuonyesha kwamba bado lipo baada ya wapiganaji wake kuangamizwa kufuatia operesheni za kijeshi.

Shambulizi hilo ni la kwanza mnamo kipindi cha miaka mitatu katika eneo hilo la msongamano wa watu mjini Bagdad.

Shambulizi lingine la aina hiyo lilifanyika mwaka 2018,muda mfupi baada ya waziri mkuu wa wakati huo Haidar al-Abadi kutangaza ushindi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu.

Mashambuli hayo ya Alhamisi yamekuja siku kadhaa baada ya serikali kutangaza kuandaa uchaguzi wa mapema mwezi Oktoba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW