1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAustralia

Idadi ya waliokufa shambulio la kisu Australia yafikia 6

13 Aprili 2024

Idadi ya waliokufa kwenye shambulio la kisu mjini Sydney nchini Australia imefikia 6 na wengine kadhaa waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu ikiwemo mtoto wa miezi tisa.

Huduma za dharura kwenye mkasa wa shambulio la kisu mjini Sydney, Australia.
Huduma za dharura kwenye mkasa wa shambulio la kisu mjini Sydney, Australia.Picha: David Gray/AFP/Getty Images

Mkasa huo kwenye mtaa wa shughuli nyingi za manunuzi umetokea pale mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 40 alipoanza kuwashambulia watu ovyo kwa kisu kabla ya mwenyewe kuuliwa kwa kupigwa risasi na polisi.

Kamanda wa polisi wa mji wa Sydney, Karen Webb, amesema waliouawa ni wanawake watano na mwanamme mmoja na waliojeruhiwa ni wanane.

Waziri Mkuu wa Australia Antony Albanese amelaani shambulio hilo  ambalo hadi sasa dhamira ya aliyelifanya haijafahamika. Mfalme Charles III wa Uingereza na mkewe Camilla ni miongoni mwa viongozi duniani waliotuma salamu za pole na rambirambi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW