1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Iran: Idadi ya walionyongwa yaongezeka na kuzua hofu

13 Aprili 2023

Mashirika mawili ya haki za binadamu yamesema Iran iliwanyonga asilimia 75 zaidi ya watu mwaka wa 2022 kuliko mwaka 2021.

Iran | Proteste am Internationalen Frauentag
Picha: bidarzani

Katika ripoti iliyotolewa na mashirika hayo Iran Human Rights IHR, lililo na makao yake Denmark na Together Against the Death Penalty ECPM, lililo na makao yake mjini Paris, huenda watu wengi zaidi wakanyongwa mwaka huu baada ya maandamano yaliyodumu kwa muda mrefu kuikumba jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Ripoti hiyo inasema watu 582 walinyongwa mwaka jana idadi hiyo ikiwa ya juu zaidi tangu mwaka 2015 na juu zaidi hata kushinda ile ya watu zaidi ya 300 walionyongwa mwaka 2021.

Soma pia:Papa Francis alaani unyongaji Iran huku wengine 3 wakihukumiwa kifo 

Mkurugenzi wa shirika la Iran Human Rights, Mahmood Amiry Moghaddam, amesema ingawa idadi ya wanaonyongwa kutokana na maandamano si kubwa, Iran inaendelea na adhabu hiyo kwa watu wanaohukumiwa kwa makosa mengine ili kuwatia hofu watu wasiandamane.