1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waomba hifadhi waliopokea msaada Ujerumani wapungua

11 Septemba 2025

Idadi ya waomba hifadhi wanaopokea malipo ya ustawi nchini Ujerumani ilipungua kwa takriban asilimia 10% kutoka 513,700 hadi 461,000 - kati ya mwisho wa mwaka 2023 na mwisho wa mwaka 2024, kulingana na takwimu rasmi.

Ujerumani | Dortmund 2015 |
Watu wakiwakaribisha wakimbizi kwa bango linalosomeka 'karibu Ujerumani' mjini Dortmund, Ujerumani baada ya maelfu ya wahamiaji kuwasili nchini humoPicha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Kupungua kwa idadi ya wapokeaji wa msaada wa serikali kulitokana na kushuka kwa idadi ya jumla ya waomba hifadhi nchini humo.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka ofisi ya takwimu ya shirikisho la Ujerumani (Destatis), asilimia 64 ya waliokuwa wakipokea malipo ya ustawi kwa sababu mwishoni mwa mwaka 2024 walikuwa wanaume na asilimia 29 walikuwa watoto wadogo.

Kwa mara ya kwanza, raia wa Uturuki waliwapita Wasyria kama kundi kubwa zaidi la wapokeaji wa misaada ya ustawi.

Wengi wa waliokuwa na haki ya kupokea malipo walitokea Uturuki (15%), Syria (14%) na Afghanistan (11%), huku raia wa Uturuki wakiwapiku Wasyria kama wapokeaji wakuu wa misaada ya serikali.

Takwimu mpya kutoka Shirika la Hifadhi la Umoja wa Ulaya zinaonyesha mabadiliko makubwa katika mtiririko wa waomba hifadhi barani Ulaya. Kwa mara ya kwanza katika zaidi ya muongo mmoja, Ujerumani haiongozi tena kwa idadi ya waomba hifadhi wapya.

Katika tathmini yake ya katikati ya mwaka 2025, shirika hilo limeeleza kwamba kulikuwepo na maombi mapya 70,000 nchini Ujerumani ya waomba hifadhi, na kuiweka nchi hiyo katika nafasi ya tatu nyuma ya Ufaransa (78,000) na Uhispania (77,000)

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW