1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wasiokua na ajira imepungua nchini Ujerumani

28 Aprili 2005
Kwa mara ya kwanza kabisa tangu zaidi ya mwaka mmoja uliopita,idadi ya watu wanaotafuta ajira imepungua humu nchini.Ofisi kuu ya Ajira imesema katika ripoti yake hii leo idadi ya wasiokua na ajira imepungua kwa watu 79 elfu na kusalia chini ya watu milioni tano.Watu milioni 4,na laki nane na 89 wamejiandikisha hawana kazi,hiyo ikiwa ni sawa na asili mia 11.8,kulinganisha na asili mia 12 mwezi uliopita..Idadi ya wasiokua na ajira iligonga rekodi mwezi februara mwaka huu walipofikia watu milioni 5 laki mbili na 16 elfu.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW