Idadi ya watu China yapungua kwa mwaka wa pili mfululizo
17 Januari 2024Takwimu zilizotolewa leo zimeonyesha kuwa nchi hiyo ya Asia Mashariki ilikuwa na idadi ya watu wapatao bilioni 1.409 kufikia mwisho wa mwaka 2023, idadi hiyo ikiwa pungufu ya watu milioni 2.08 kutoka mwaka 2022.
Pia, idadi ya vifo vilivyoripotiwa mwaka jana viliongezeka kwa asilimia 6.6, sawa na watu milioni 11.1, kiwango hicho kikiwa cha juu zaidi tangu mwaka 1974 wakati wa mapinduzi ya utamaduni.
China yatangaza kupungua kwa idadi ya watu wake
Hata hivyo, wataalamu wanatoa hoja kwamba upungufu huo wa idadi ya watu ulitarajiwa kutokana na kuongezeka kwa tabaka la watu wanaoishi mjini na pia kiwango kidogo cha watoto wanaozaliwa.
China imeshuhudia kiwango kidogo cha watoto wanaozaliwa kwa miongo kadha sasa- hasa baada ya kuweka sera yenye utata ya kuwataka watu kuwa na mtoto mmoja tu.