1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya watu kufikia bilioni 9.7 duniani

Sekione Kitojo
18 Juni 2019

Idadi ya watu duniani inatarajiwa kufikia bilioni 9.7 ifikapo mwaka 2050 kutoka idadi ya watu bilioni 7.7, ambapo idadi ya watu katika eneo  la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara ikiongezeka maradufu.

Liberia Jewel Cianeh Howard Taylor
Picha: Getty Images/AFP/G. Gobet

Idadi  ya  watu  duniani  inakuwa  na  wazee  zaidi na  ukuaji  ni  kwa kasi  ndogo lakini  bado  inatarajiwa  kuongezeka  kutoka  idadi ya sasa  ya   watu  bilioni 7.7  hadi  kufikia  bilioni 9.7 ifikapo  mwaka 2050. Idara ya  Umoja  wa  mataifa  ya  masuala ya  uchumi  katika kitengo  cha  idadi  ya  watu imesema  katika  ripoti  kwamba  idadi ya  watu  inaweza  kufikia kiwango chake  cha  juu  cha  karibu  watu bilioni 11 kuelekea  mwishoni  mwa  karne hii.

John Wilmoth mkurugenzi wa idara ya idadi ya watu ya Umoja wa MataifaPicha: Imago Images/Xinhua/X. Xiaolei

Lakini mkurugenzi wa  idara  ya  idadi  ya  watu  John Wilmoth ameonya  kuwa  kwasababu  mwaka  2100 uko mbali kwa miongo mingi bado ,matokeo  haya  "hayana  hakika" ,  na  mwishoni kiwango  cha  juu  kinaweza  kuja  mapema  ama  baadaye,  katika kiwango  cha  juu  ama  cha  juu  cha  jumla  ya  idadi  ya  watu."

Utabiri mpya  wa  idadi ya  watu  unaonesha  kuwa  nchi  tisa zitahusika  na  zaidi  ya  nusu  ya  ukuaji  unaotabiriwa  wa  idadi  ya watu  kati  ya  hivi  sasa   na  mwaka  2050.

Idadi ya viwango vya uzazi vinapunguaPicha: Getty images/AFP Photo/P. U Ekpei

Nchi wachangiaji wa idadi ya watu

Nchi  ambazo zitahusika  na kuiongezea  dunia  idadi kubwa ya  watu kuanzia  ile ya  juu  hadi  ya  chini  ni  pamoja  na  India , Nigeria, Pakistan, Congo, Ethiopia, Tanzania, Indonesia, Misri  na  Marekani.

Katika  eneo  la  Afrika  kusini  mwa  jangwa  la  Sahara , idadi  ya watu  inakadiriwa  kuongezeka  maradufu  ifikapo  mwaka  2050, ripoti  hiyo  imesema.

Idadi ya watu kusini mwa jangwa la Sahara itapanda zaidi kwa kasi zaidi hadi 2050Picha: picture-alliance/NurPhoto/M. Moskwa

Msaidizi  wa  katibu  mkuu  anayehusika  na  uchumi  na  masuala ya  jamii  Lu Zhenmin  amesema  katika taarifa, kwamba  "Nyingi  ya nchi zenye  ukuaji  mkubwa  wa  idadi  ya  watu  ziko  katika   mataifa masikini, ambako  ukuaji  wa  idadi  ya  watu  unaongeza changamoto  katika  juhudi  za  kufuta  ujinga," kuhimiza usawa  wa kijinsia  na  kuwezesha  hali  bora  ya  huduma  za  afya na  elimu.

Ripoti  hiyo  inathibitisha  kuwa  idadi  ya  wazee duniani inaongezeka kutokana  na kupanda kwa kiwango cha matarajio ya kuishi na  kupungua kwa  viwango vya  uzazi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW