1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya maiti zilizofukuliwa Shaka hola yapindukia 400

18 Julai 2023

Idadi ya watu waliokufa kuhusiana na kundi linalohubiri mwisho wa dunia imepindukia 400, baada ya miili mingine 12 kufukuliwa jana, inayoaminika kuwa ya wafuasi wa mchungaji aliewaamuru kufunga hadi kufa

Zoezi la kufukua maiti zinazoaminika kuwa za wafuasi wa kanisa la Good News International katika kaunti ya Kilifi nchini Kenya
Zoezi la kufukua maiti katika kaunti ya Kilifi nchini KenyaPicha: Stringer/REUTERS

Mchungaji Paul Mackenzie, ambaye anahusishwa na kundi hilo lililokuwa na makao yake kwenye eneo la msitu katika kaunti ya Malindi, Pwani ya Kenya, yuko mikononi mwa polisi pamoja na washukiwa wengine 36. Kamishna wa mkoa wa Pwani Rhoda Onyancha, alisema jana kuwa idadi ya waliokufa imefikia 403, na watu 95 wameokolewa.

Waliookolewa waligomea kula

Mwezi uliyopita, baadhi ya washukiwa na watu waliookolewa walianzisha mgomo wa njaa gerezani na kwenye kituo cha uokozi, na kumlazimisha mwendesha mashtaka kuwapeleka mahakamani kwa mashtaka ya kujaribu kujiua. Wengi wao walikubali kuanza tena kula lakini mshukiwa mmoja alikufa akiwa kizuwizini.

Watu wapatao 613 waripotiwa kupotea

Watu wapatao 613 wameripotiwa kupotea kwa maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya walioko mjini Malindi, na maafisa wa uchunguzi wanaendelea kugundua makaburi zaidi ya halaiki.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW