1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya watu waliouwawa katika Ukanda wa Gaza yafikia 100

23 Februari 2024

Idadi ya waliouwawa kwa makombora ya Israel kipindi cha masaa 24 katika Ukanda wa Gaza imefikiwa watu 100, huku kukiwa na ripoti mbaya za ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Ukanda wa Gaza | Mawingu ya moshi juu ya Khan Yunis
Picha hii iliyopigwa kutoka Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza inaonyesha moshi ukifuka wakati wa shambulio la bomu la Israel dhidi ya Khan Yunis mnamo Februari 22, 2024,Picha: SAID KHATIB/AFP/Getty Images

Duru za sasa kwa mujibu wa Wizara ya Afya ambayo ipo chini ya mamlaka ya Hamas katika eneo la Gaza inasema zaidi ya Wapalestina 100 wameuwawa katika mashambulizi ya Israel kwenye Gaza Ukanda katika kipindi cha masaa 24.

Kwa idadi hiyo sasa jumla watu waliuwawa Gaza imefikia 29,514. Taarifa ya wizara hiyo iliongeza kwa kusema watu wengine 69,616 wamejeruhiwa tangu kuzuka kwa mapigano Oktoba 7.

Kiongozi wa Hamas ameondoka nchini Misri

Awali taarifa ya Hamas ilisema kiongozi wake Ismail Haniyeh alifanya mazungumzo na Misri kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano huko Gaza na kubadilishana mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Wapalestina waliofungwa Israel.

Wanawake na watoto wa Kipalestina wakitazama waliposimama kwenye muundo wa jengo lililoharibiwa sana tarehe 22 Februari 2024.Picha: MOHAMMED ABED/AFP/Getty Images

Katika hatua inyaofanana na hiyo, ujumbe wa Israel ukiongozwana mkuu wa shirika la kijasusi la nchi hiyo upo mjini Paris kwa ajili ya kuanzisha mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Gaza. Taarifa zinasema mkurugenzi wa shirika hilo-Mossad, David Barnea ataungana na mwenzake katika wakala wa usalama wa Shin Bet, Ronen Bar.

Usitishaji vita wa wiki moja wa mwishoni mwa Novemba ulisababisha kuachiliwa kwa mateka zaidi ya 100 waliochukuliwa na wanamgambo wa Hamas na wafungwa 240 wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa na  Israel. Mwishoni mwa Januari, Barnea alikuwa Paris na wenzake wa Marekani na Misri pamoja na waziri mkuu wa Qatar kujadili usitishaji mpya wa mapigano.

Mipango isiyo na uhakika wa makubaliano ya kusitisha mapigano

Chanzo cha Hamas kilithibitisha mpango huo uliiopendekeza kusitishwa kwa wiki sita katika mzozo huo na kuachiliwa kwa wafungwa kati ya 200 na 300 wa Kipalestina kwa kubadilishana na mateka  kati ya mateka 35 hadi 40 ambao bado wanashikiliwa na Hamas.

Hamas inataka usitishaji kamili wa mapigano na kuondolewa kwavikosivya Israel kutoka Gaza lakini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepuuzilia mbali matakwa hayo na kuyataja kuwa ya "ajabu". Amesema serikali yake iko tayari kusitisha mapigano ingawa aliapa kuendelea na mashambulizi hadi "ushindi kamili" na kulivunja nguvu kabisa kundi la Hamas.

Huko Geneva ripoti ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo ilibainisha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na pande zote nchini Israel na upande wa Palestina, na kutaka uwajibikaji na haki ili kudumisha amani.

Soma zaidi:Watu 71 wauawa katika mashambulizi kusini, katikati mwa Gaza

Mkuu wa ofisi ya Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk amesema kumekuwa na ukosefu wa kuadhibiwa uliokithiri, hali ambayo haiwezi kuruhusiwa kuendelea. Lazima kuwe na uwajibikaji kwa pande zote kwa ukiukaji unaoonekana kwa miaka 56 ya uvamizi na miaka 16 ya kuzingirwa kwa Gaza, na hadi leo.

Ndani Israel, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewasilisha mpango wake wa utawala wa gaza baada ya vita. Mpango huo unataka jeshi la Israel kudhibiti kikamilifu pwani yote ya Gaza.

Vyanzo: AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW