Idadi ya watu waliouwawa Mogadishu yaongezeka
15 Oktoba 2018Idadi ya watu waliouwawa katika shambulizi la miripuko miwili ya mabomu kwenye mikahawa miwili mjini Baidoa nchini Somalia mwishoni mwa juma lililopita, imefikia 20 na wengine 40 kujeruhiwa.
Duru zimeeleza kuwa washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walijiripua katika shambulizi la mapema Jumamosi asubuhi. Kundi la al-Shabaab limedai kuhusika na shambuliozi hilo. Msemaji wa kundi hilo amesema wameulenga mkahawa huo kwa sababu ni mahala ambako wanajeshi huwepo kila mara.
Jumapili ilitimia mwaka mmoja, tangu shambulizi la bomu katika mji mkuu wa Somalia-Mogadishu, ambalo linashukiwa lilifanywa pia na Al-Shabaab, lilipowauwa watu zaidi ya 500.
Mahakama ya kijeshi ya Somalia, ilimhukumu adhabu ya kifo mtu mmoja aliyekutikana na hatia ya kuhusika katika shambulizi hilo.