1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya watu wasio na ajira Ujerumani yaongezeka mwezi Juni

28 Juni 2024

Idadi ya wasiokuwa na ajira nchini Ujerumani imeongezeka hadi watu milioni 2.72 mwezi huu wa Juni. Idadi hiyo ni ongezeko la watu 4,000 tofauti na mwezi uliopita.

Ujerumani |  Kansela Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Ronny Hartmann/AFP/Getty Images

Shirika la serikali linalohusika na takwimu kuhusu ajira limesema kulikuwepo na watu 172,000 wasiokuwa na ajira mwaka uliopita. 

Soma pia:Wafanyakazi wahamiaji wanahofia ubaguzi wa rangi Ujerumani?

Shirika hilo limeeleza kuwa, janga la ugonjwa wa UVIKO-19, ujio wa wakimbizi kutoka Ukraine na uchumi kutetereka ni baadhi ya sababu za kuongezeka kwa kiwango cha ukosefu wa ajira.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW