MigogoroIsrael
IDF lashambulia "miundombinu ya kijeshi" ya Hezbollah
30 Novemba 2024Matangazo
Taarifa ya jeshi imesema ndege zake zilishambulia maeneo hayo yanayotumika kusafirisha silaha kutoka Syria hadi Lebanon.
Katika hatua nyingine, wanamgambo hao wa Hezbollah hii leo wanafanya kumbukumbu ya kiongozi wao aliyeuliwa na Israel, Hassan Nasrallah.
Nasrallah aliuawa Septemba 27, katika makao makuu ya kundi hilo na kumbukumbu hiyo inafanyika kusini mwa Beirut, ambako ni ngome ya Hezbollah.