1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IEBC yatoa mafunzo kwa waandishi kuelekea uchaguzi

Wakio Mbogho14 Juni 2022

Tume ya uchaguzi ya Kenya, IEBC inafanya majadiliano na kutoa mafunzo kwa wanahabari nchini kote kuhusu jukumu lao katika kuripoti juu ya uchaguzi ujao, hasa makosa ya kiteknolojia na njjia za kuhakiki ukweli wa taarifa.

Kenia Kalobeyei  | Taphine Otieno - Content Development Coordinator
Picha: FilmAid Kenya

Majadiliano kati ya wanahabari kutoka maeneo mbalimbali nchini Kenya na maafisa wa tume ya IEBC yamekamilika hii leo mjini Nakuru baada ya mafunzo ya siku tatu. Kulingana na Hillary Kombe, afisa katika tume hiyo, wanalenga kusahihisha ripoti na dhana potofu zinazoenezwa kuhusu mchakato wa uchaguzi kwa kuhakikisha kwamba, wanahabari wanaotambulika kama kioo cha jamii wamepata ufahamu unaofaa.Tume ya IEBC Kenya yafanyia majaribio mfumo wake wa matokeo

Naibu Rais William Ruto na viongozi wanaounga mkono mrengo wake wamelalamikia mipango ya serikali kuiba uchaguzi kwa kuwa wanampendelea mpinzani wake Raila Odinga.

Waandishi wa habari wakiandamana NairobiPicha: imago stock&people

Mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati alitangaza kwamba uchaguzi mkuu ujao utaendeshwa kwa njia ya kielektroniki pekee, kinyume na awali ambapo mbinu zote, ya kisasa na ya zamani zilitumika. Kumekuwa na wasiwasi kuhusu matumizi ya mbinu ya teknolojia pekee ikizingatiwa kuwa baadhi ya maeneo hayana miundo mbinu yenye uhakika. Hata hivyo, IEBC imetoa hakikisho kwamba wametambua palipo huduma mbalimbali za mitandao kama vile 2G na 4G na tayari wameweka mikakati kuwezesha usambazaji wa matokeo ya uchaguzi.Tume ya uchaguzi Kenya yapendekeza mabadiliko.

Pamoja na hayo, waandishi wa habari wamepata ufahamu kuhusu namna ya kuhakikisha wanaripoti taarifa zilizosahihi, na kuepuka habari potofu ambazo zimeenezwa sana kwenye mtandao wa kijamii. Michael Wachira mwanachama wa muungano wa wahariri nchini Kenya anashauri kwamba kulingana na sheria, mwandishi wa habari anapochapisha taarifa za uongo ni hatia na haijalishi hata kama matamshi hayo yalisemwa kwenye mkutano fulani.

Mara hii Tume ya IEBC italazimika kuzingatia maelezo ya afya kuhusu kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 ikizingatiwa kuwa maambukizi yanaripotiwa kuongezeka. Aidha, vifaa vya kielektroniki vitakavyokuwa vinatumiwa ni vichache mno na vitatumiwa na watu wengi.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW