IGAD yaahirisha mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini
19 Aprili 2018Jumuiya ya ushirikiano wa nchi za pembe ya Afrika IGAD imesema kuwa imeahirisha mazungumzo ya mwezi huu yanayolenga utekelezaji wa mkataba wa amani wa Sudan Kusini ikiwa ni hatua ya hivi karibuni ya kukomesha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu nchini humo kwa miaka minne.
Licha ya makubaliano kadhaa pamoja na usitishwaji mapigano bado mgogoro nchini Sudan Kusini umekuwa ukiendelea tangu mapigano yalipoibuka mwishoni mwa 2013 ikiwa ni miaka miwili baada ya nchi hiyo kupata uhuru. Jumuiya ya IGAD iliyokuwa inatarajiwa April 26 kuwa na mazungumzo mapya pamoja na vyombo vingine vya kimataifa kuhusiana na utekelezaji wa mkataba huo imekuwa ikitafuta njia ya kupatikana suluhu kati ya pande mbili zinazozozana nchini humo ikiwa ni pamoja na kuachiwa kwa kiongozi wa waasi Riek Machar.