Kim Jong Un kuzuru Moscow hivi karibuni
11 Septemba 2023Minong'ono imekuwa ikiongezeka katika siku za hivi karibuni kwamba KimJong Unambaye hutoka mara chache nchini mwake na ambaye hajasafiri tangu enzi ya janga la UVIKO-19, anatarajiwa kukutana na Putin kujadiliana makubaliano muhimu ya silaha.
"Kufuatia mwaliko wa rais Vladimir Putin wa Urusi, Kim Jong Un, Mwenyekiti wa Masuala ya Kitaifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea atazuru Shirikisho la Urusi katika siku zijazo," imesema Ikulu ya Moscow, Kremlin.
Shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap liliripoti mapema kwamba treni ya Kim Jong Un huenda tayari imeondoka kwenda Urusi, ikimnukuu afisa mmoja ambaye hakutambulishwa.
Urusi ambaye ni mshirika wa siku nyingi wa Pyongyang alikuwa ni muungaji mkono mkubwa wa taifa hilo lililotengwa kwa muda mrefu na hasa kutokana na shughuli zake za nyuklia, na mahusiano baina yao yanaanzia kuasisiwa kwa Korea Kaskazini miaka 75 iliyopita.
Mwezi Julai, Putin alisifia uungaji mkono huo katika kile ambacho Urusi inachokitaja kama operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine.