1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiNigeria

IMF kutoa dola milioni 70 za ufadhili kwa Niger

Saleh Mwanamilongo
2 Juni 2024

Shirika la Fedha la Ulimwenguni IMF limetangaza kufikia makubaliano ya awali na Niger kuhusu ufadhili wa miradi kadhaa ya maendeleo.

Shirika la IMF kufadhili miradi ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi Niger
Shirika la IMF kufadhili miradi ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi NigerPicha: Liu Jie/Xinhua/IMAGO

Shirika la Fedha la Ulimwenguni IMF limetangaza kufikia makubaliano ya awali na Niger kuhusu ufadhili wa miradi kadhaa ya maendeleo. Hatua hiyo inaufungua mlango kwa ufadhili wa zaidi ya dola milioni 70 kwa taifa hilo la Sahel.  Taarifa ya shirika la IMF imesema mkataba huo utahitaji kuidhinishwa na bodi ya wakurugenzi wake, ambayo inatazamiwa kukutana mwezi ujao.

Makubaliano baina ya shirika la IMF na nchi ya Niger yanahusu pia miradi ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi. Shirika la IMF ni miongoni mwa taasisi chache zinazoendelea kutoa msaada kwa Niger, ambayo rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazouma alipinduliwa mwaka jana katika mapinduzi ya kijeshi.

Marekani, Umoja wa Ulaya, Ufaransa na Ujerumani zimesitisha pragramu kadhaa za msaada kwa Niger, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani. Kwa upande wake, Benki Kuu ya Dunia ilitangaza katikati ya mwezi wa Mei kuanza tena ufadhili wa miradi kadhaa nchini Niger.