IMF: Mabadiliko ya tabia nchi huenda yakaongeza vifo
30 Agosti 2023Katika ripoti yake iliyochapishwa leo, IMF inasema matukio ya kimazingira tu hayawezi kuchocheamizozo ila yanaweza kufanya hali zinazojitokeza kwenye mizozo kama njaa, umaskini na watu kuachwa bila makao, kuwa mbaya zaidi.
Ripoti hiyo inasema ifikapo mwaka 2060, vifo vinavyotokana na mizozo huenda vikaongezeka kwa asilimia 8.5.
Soma pia:Wanasayansi wajadili zaidi juu ya mabadiliko ya hali ya hewa
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, nchi ambazo zitaathirika zaidi ni zile zinazokabiliwa na mizozo na hali tete na huenda vifo vikaongezeka kwa hadi asilimia 14 katika mataifa yanayokabiliwa na ongezeko la joto.
Shirika hilo la fedha duniani limeonya kuwa, watu milioni 50 zaidi katika nchi hizo huenda wakakabiliwa na njaa kutokana na uzalishaji mdogo wa chakula.