IMF yaipa Burkina Faso mkopo wa dola milioni 302
22 Septemba 2023Matangazo
IMF imesema mkopo huo utaipa Burkina Faso nafasi ya kuyatekeleza matumizi yake ya kipaumbele baada ya nchi hiyo kukabiliwa na mapinduzi mara mbili tangu mwezi Januari mwaka jana.
Burkina Faso pia inakabiliwa na hali mbaya ya usalama na kiuchumi iliyochangiwa na vita vya nchini Ukraine, misukosuko iliyosababishwa na janga la COVID-19, ukame, migogoro na uhaba wa chakula.
Soma: Ibrahim Traore kuapishwa Ijumaa kama rais wa mpito
IMF imesema majanga hayo yamevuruga uchumi na ustawi katika taifa hilo la Afrika magharibi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linakadiria kuwa zaidi ya watu milioni mbili wamegeuka kuwa wakimbizi wa ndani kutokana na kutokuwepo kwa usalama nchini Burkina Faso.