1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurundi

IMF yakubali kuikopesha Burundi baada ya miaka minane

11 Aprili 2023

Shirika la Kimataifa ya Fedha, IMF, imekubali kuikopesha Burundi Dola milioni 261.7, ukiwa ni mkopo wa kwanza katika kipindi cha miaka minane, katika jaribio la kuhamasisha ufufuaji na mageuzi ya uchumi.

Präsident der Republik Burundi Evariste Ndayishimiye in Kinshasa
Picha: Giscard Kusema/Pressedienst der Präsidentschaft des Kongo

Makubaliano hayo ya ngazi ya wataalamu yalifikiwa katika ziara ya timu ya IMF katika mji mkuu Bujumbura. Mkopo huo hata hivyo bado utahitaji kuidhibishwa na utawala wa IMF.

Burundi imekuwa katika mzozo wa kiuchumi tangu mvutano mbaya wa kisiasa wa mwaka 2015, huku ikikabiliwa na upungufu wa fedha za kigeni na bidhaa muhimu. Mzozo huo ulichochewa zaidi na janga la UVIKO-19 na vita vya Ukraine.