1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMorocco

IMF yalazimisha ufadhili kupambana na umasikini

Josephat Charo
13 Oktoba 2023

Shirika la IMF na Benki ya Dunia yahimiza ufadhili kupambana na umasikini na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Marokko | Treffen des Internationalen Währungsfonds in Marokko | Präsident der Weltbankgruppe (WBG) Ajay Banga
Picha: Abu Adem Muhamme/AA/picture alliance

Mkuu wa shirika la fedha la kimataifa IMF Kristalina Georgieva na rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga wamezihimiza nchi wanachama ziimarishe ufadhili wa fedha kwa mashirika hayo ya wakopeshaji wanaoongoza kuzisaidia nchi masikini kupambana na umasikini na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakuu hao wametoa wito huo katika mkutano unaowakutanisha mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu mjini Marrakesh nchini Morocco, mkutano wa kwanza wa IMF na Benki ya Dunia unaofanyika barani Afrika tangu 1973.

Banga amesema maendeleo katika mapambano dhidi ya umasikini yanadidimia, ulimwengu unakabiliwa na mgogoro wa mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa usalama wa upatikanaji wa chakula, kuyumba kwa uchumi, harakati za kujinasua kutokana na athari za janga la corona na athari za mizozo mbali na uwanja wa vita.