1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMamlaka ya Palestina

IMF: Ukuaji wa chumi za Mashariki ya Kati kushuka 2024

11 Februari 2024

Shirika la Fedha Duniani IMF, limesema kuwa chumi za mataifa ya Mashariki ya Kati ziko chini ya makadirio ya ukuaji kutokana na kupunguzwa kwa uzalishaji wa mafuta na mzozo wa Israel wa Ukanda wa Gaza

Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano na wenye viti wa mashirika matano makubwa ya kiuchumi duniani pamoja na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Mkuu wa IMF Kristalina GeorgievaPicha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Mkuu wa shirika hilo la IMF Kristalina Georgieva, ameliambia Jukwaa la Sera za Uchumi kwa mataifa ya kiarabu linalofanyika mjini Dubai kwamba licha ya hali zisizotabirika,uchumi wa dunia umesalia kuwa himilivu, huku akionya kuhusu uwezekano wa athari kubwa zaidi kwa chumi za kanda ya Mashariki ya Kati kutokana na mzozo unaoendelea katika Ukanda huo wa Gaza.

Chumi zinazopakana na Israel na maeneo ya Palestina zashuhudia athari za mzozo wa Gaza

Georgieva amesema, chumi za mataifa yanayopakana na Israeli na maeneo ya Palestina zimeshuhudia mzozo huo ukiathiri mapato yanayotokana na utalii huku mashambulizi katika Bahari ya Shamu yakiathiri gharama za usafirishaji mizigo kimataifa.

Soma pia:IMF: Ukuaji uchumi duniani kushuka kwa 3% mwaka 2023

Georgieva, ameliambia jukwaa hilo pembezoni mwa  mkutano wa kilele wa wakuu wa serikali duniani mjini Dubai kwamba masuala hayo yameongezea changamoto za chumi ambazo bado zinafufuka kutokana na misukosuko ya awali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW