1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan azuiwa kugombea urais

31 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan aleyeko gerezani Imran Khan amezuiwa kugombea katika uchaguzi ujao, sambamba na wafuasi wake wengi, maafisa wa chama chake wamesema baada ya kufungwa kwa mchakato wa uteuzi.

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani Imran Khan katika moja ya mikutano na waandishi wa habari katika makazi yake huko Lahore, Pakistan Mei 18, 2023.Picha: Mohsin Raza/REUTERS

Tume ya Uchaguzi ya Pakistan, ECP ilimuengua Imran Khan baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi, lakini chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kiliwasilisha nyaraka zake za uteuzi wiki iliyopita kikipuuzia mbali hatua hiyo.

Msemaji wa (PTI), Raoof Hasan amesema asilimia 90 hadi 95 ya nyaraka za wagombea wao zimekataliwa.

Afisa mmoja wa tume ya uchaguzi amelithibitishia shirika la habari la AFP juu ya hatua hiyo, akisema imezingatia hatia dhidi ya wagombea hao ambao ni pamoja na Khan. Orodha ya wagombea wa mwisho itatangazwa Januari 23.

Khan amekuwa gerezani tangu mwezi Agosti akikabiliwa na msururu wa kesi ambazo anasisitiza zimechochewa ili kumzuia kuwania kwenye uchaguzi huo unaofanyika Februari 8, mwaka 2024.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW