1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Imran Khan na mkewe wahukumiwa miaka mingine 7 gerezani

3 Februari 2024

Mahakama ya Pakistani leo hii imemtia hatiani na kumhukumu Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan na mkewe kifungo kingine cha hadi miaka saba gerezani kwa madai kwamba ndoa yao ya mwaka 2018 ilikiuka sheria.

Pakistan | Bushra Bibi auf dem Weg zur Anhörung | Archivbild Dezember 2023
Picha: Anjum Naveed/AP Photo/picture alliance

Upande wa mashtaka ulisema Khan na mkewe walikiuka sheria inayosema mwanamke lazima asubiri miezi mitatu kabla ya kuolewa tena.Hukumu hiyo inafuatia kesi nyingine ya Jumatano iliyopita ambayo Khan na mkewe, Bushra Bibi, walihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela kwa makosa ya rushwa.Hukumu hiyo inatolewa kabla ya uchaguzi wa wabunge wa Februari 8 ambao Khan tayari ameondolewa kwa sababu ya kukutwa kwake na hatia ya makosa ya ufisadi. Khan na familia yake wanasisitizakuwakesi hiyo imechochewa kisiasa. Hukumu hiyo ni ya nne kwa Khan, tangu alipoondolewa madarakani mwaka 2022.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW