1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India: Makampuni yakabiliwa na mashambulizi ya mtandaoni

Saleh Mwanamilongo
3 Oktoba 2024

India imekuwa ikikabiliana na ongezeko la mara kwa mara la mashambulizi ya mtandaoni yanayolenga biashara, benki na huduma za umma. Taasisi na makampuni yanatakiwa kuboresha zaidi miundombinu yake juu ya ulinzi wa data.

Udukuaji na mashambulio ya mtandaoni.
moja ya ishara zinazotumika kuelezea udukuaji na mashambulio ya kimtandao.Picha: SalamPix/abaca/picture alliance

Idara nyingi za serikali na sekta ya teknolojia ni miongoni sekta muhimu zinazolengwa na mashambulio ya hivi karibuni ya uombaji fidia mtandaoni nchini India. Huku huduma za afya, benki, utengenezaji na biashara ya mtandaoni pia zikiathiriwa.

Aina ya kawaida ya mashambulizi ya mtandaoni hutumia programu ya usimbaji fiche, ambayo husimba data ya mwathiriwa kwa njia fiche na kudai fidia kuptitia ufunguo maalum.

Kulingana na ripoti iliyotolewa mnamo Julai na kampuni ya kimataifa ya usalama wa mtandao ya Check Point, India ilishuhudia ongezeko la mwaka hadi mwaka la asilimia 46 ya jumla ya mashambulizi ya mtandao katika robo ya pili ya mwaka huu wa 2024.

Katika tukio moja la mapema mwezi Agosti, benki ndogo 300 za India zililazimika kufunga mifumo ya malipo ya mtandaoni kwa siku moja kutokana na shambulio la kuomba fidia mtandaoni dhidi ya kampuni ya kutoa huduma ya IT C-Edge Technologies.

Soma pia:Kenya inavyopambana kuwalinda watumiaji wa mitandao

Katika tukio kubwa mwaka jana, wadukuzi waliishambulia Taasisi ya Sayansi ya Tiba ya All India huko Delhi, na kusababisha kuzimwa kwa seva na kutatiza huduma za afya.

Mnamo mwaka wa 2019, majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh yalilengwa na shambulio la kuomba fidia mtandaoni ambalo lilitatiza mifumo ya matumizi ya umeme.

Ripoti nyingine ya hivi karibuni ya kampuni ya usalama wa mtandaoni ya Sophos ilionyesha kuwa athari za mashambulizi hayo kwa makampuni ya India yameongezeka zaidi, na mahitaji ya fidia na gharama zinaongezeka mwaka hadi mwaka. 

Ripoti hiyo pia iligundua kuwa asilimia 65 ya wale walioathirika na mashambulio ya kuomba fidia mtandaoni walikuwa na mwelekeo wa kulipa fidia ili kurejesha data. Na wastani wa ulipaji fidia ulikuwa wa dola milioni 5 milioni.

Wataalamu: Hatua za kiusalama zinahitajika haraka

Wataalamu wa mitandao na wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, TEHAMA waliiambia DW kwamba idadi ya makampuni ya India yanayokabiliwa na mashambulizi kama hayo itaongezeka isipokuwa hatua madhubuti za usalama wa mtandao zitawekwa ili kulinda taarifa nyeti.

Siku ya Mitandao Salama, hali ikoje kwa vijana Tanzania?

02:59

This browser does not support the video element.

Milind Dewanji mkurugenzi wa Pace Computers, kampuni ya huduma ya vifaa vya TEHAMA aliiambia DW kwamba Kampuni hazizingatii sera zao za TEHAMA.

Uwekezaji tu na uhamiaji kwenye huduma za miundombinu ya kimtandao kwa sera za ndani hautoshi. Amesema makampuni yamekuwa yakipuuza waziwazi mahitaji yanayohitajika, na kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu.

Dewanji aliongeza kuwa jukumu la Afisa Mkuu wa Habari (CIO) limekuwa muhimu zaidi, na kwamba vitisho vya mtandao vinapaswa kuchukuliwa kwa uzito katika ngazi ya usimamizi.

Soma pia:Meta, TikTok na X, wabanwa kuhusu usalama mtandaoni

Vishal Vasu, mkurugenzi na afisa mkuu wa teknolojia wa Dev Information Technology, kampuni ya huduma za TEHAMA alidokeza kuwa wahalifu wa mtandao wanazidi kuongeza mashambulizi, wakitumia teknolojia na udhaifu wa mifumo wa makampuni.

Mashambulizi dhidi ya biashara ndogo ndogo na biashara za kati ambayo ni muhimu kwa uchumi wa India, yamekuwa sababu ya wasiwasi mkubwa nchini humo.

Kwa kuzingatia kwamba biashara hizo huchangia zaidi ya asilimia arobaini ya jumla ya mauzo ya nje ya India, wengi wanahisi ni muhimu kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza hatari ya mashambulizi ya kuomba fidia mtandaoni.