1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Je, muungano mpya India unaweza kumuondoa Modi 2024?

25 Julai 2023

Zaidi ya dazeni mbili ya vyama vya upinzani vimeweka kando tofauti zao na kuuda muungano wa upinzani dhidi ya chama cha Bharatiya Janata cha waziri mkuu wa India Narendra Modi katika uchaguzi ujao wa bunge mwakani.

Indien | Treffen der Oppositionsparteien in Bengaluru
Picha: Indian National Congress

Viongozi wa vyama 26 vya upinzani nchini India walikusanyika wiki iliyopita ili kuunda muungano mpya kupambana na chama tawala cha Waziri Mkuu Narendra Modi cha Bharatiya Janata Party (BJP) katika uchaguzi wa bunge unaotarajiwa mwaka ujao.

Muungano huo mpya - unaoitwa Indian National Developmental Inclusive Alliance (INDIA) - ulisema katika taarifa kwamba BJP ilikuwa ikiharibu sifaya jamhuri. Waliahidi "kulinda wazo la India kama ilivyoainishwa katika Katiba."

"Tunaweka kando tofauti zetu za kisiasa ili kuokoa demokrasia. Lengo kuu ni kusimama pamoja kulinda demokrasia na katiba," alisema Mallikarjun Kharge, rais wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Congress.

Soma pia:India: Rahul Gandhi apoteza kiti chake cha Bunge

Wakosoaji wanasema tangu BJP ilipoingia madarakani mwaka 2014, imekuwa ikifuata ajenda ya uzalendo wa kitaifa ya Kihindu na kusababisha mgawanyiko katika jamii ya Wahindi katika misingi ya kidini.'Lakini BJP inashikilia kuwa inawakilisha Wahindi wote na kwamba inataka ukuaji kwa wote.

Muungano mpya wa upinzani unajumuisha Congress pamoja na safu ya vyama vyenye nguvu vya kikanda, kama vile chama cha Aam Aadmi, ambacho kinatawala Punjab na Delhi, na Trinamool Congress, ambacho kiko madarakani katika jimbo la mashariki la Bengal Magharibi.

Kiongozi wa Congress Rahul Gandhi aliuelezea uchaguzi wa mwaka ujao kama "mapambano kati ya Narendra Modi na INDIA."

Upinzani wa pamoja dhidi ya BJP

Zoya Hasan, mwanasayansi wa siasa, alisema kuwa "ni maendeleo muhimu sana ya kisiasa."

"Taarifa iliyotolewa na vyama hivi inatoa simulizi mbadala iliyoegemezwa katika wazo la kikatiba la India lenye msingi wa demokrasia ya kilimwengu, mamlaka ya kiuchumi, haki ya kijamii, na shirikisho," aliiambia DW.

wapiga kura wakiwa katika msururu wa kwenda kupiga kura katika uchaguzi mdogo mwezi Mei.Picha: STRINGER/REUTERS

Hasan alisema itakuwa vigumu kwa BJP kushindawingi wa viti bungeni katika uchaguzi ujao "ikiwa vyama vya upinzani vinaweza kuendeleza kasi hiyo." Lakini mtaalam huyo alidokeza kuwa muungano huo mpya una kazi kubwa ya kufanya.

"INDIA haiwezi tu kuwekea kikomo zoezi la urekebishaji wa viti, inapaswa kuhamasisha uungwaji mkono maarufu kwa mjadala mbadala," aliongeza.

Vyama vingi katika muungano huo mpya ni wapinzani wa kikanda na vimegawanyika katika ngazi ya kitaifa. Lakini sasa wamejaribu kuweka kando tofauti zao ili kukabiliana na BJP, ambayo inasalia kuwa maarufu na inaonekana kuwa na uwezo wa kushinda uchaguzi ujao.

Soma pia:Watu 7wauwawa kwenye fujo za uchaguzi wa serikali za mitaa India

Kharge, rais wa chama cha Congress, alisema mkutano ujao wa muungano huo utaunda jopo la uratibu na kuitisha mkongamano. Utashughulikia pia suala tata la kugawanya viti kwa vyama katika muungano kugombea moja kwa moja dhidi ya BJP.

"Vyama vikuu vya upinzani vina uwezekano wa kupitisha kiolezo kipya cha Misheni 2024 na kuzingatia maswala muhimu ya kitaifa pamoja na yale mahususi ya serikali kukabiliana na BJP," kiongozi mashuhuri wa Congress aliiambia DW. "BJP imenufaika kwa jadi katika mpambano wa pembetatu na itakuwa inaangalia mpambano wa ana kwa ana."

Chama cha Congress hivi karibunikilipata msukumo baada ya kuiondoa BJP katika jimbo la kusini la Karnataka mwezi Mei. Kinatumai changamoto ya umoja wa upinzani itafaulu kumzuia Modi kupata muhula wa tatu mnamo 2024.

Je, BJP inautazamaje muungano huo mpya?

BJP, wakati huo huo, imepuuza umuhimu wa muungano mpya. Chama na Modi pia kilikosoa vyama vya upinzani kikivitaja kama wabinafsi na mafisadi  ambao wameikashifu India ulimwenguni lakini sasa walikuwa wakijaribu kuokoa uwepo wao na familia zao.

Maelfu waandamana kupinga sheria tata ya uhamiaji India

01:10

This browser does not support the video element.

Waziri Mkuu alisema kwamba miungano ya kisiasa "iliyojengwa juu ya uhasi" haikufaulu kamwe. "Tunaunganisha watu wa India, wanagawanya watu wa India, wanadharau watu wa kawaida wa India," alisema, akimaanisha vyama vya upinzani.

"Ushirika wa (INDIA) ni mtoto aliyezaliwa mfu na hata madaktari hawajui jinsi ya kumwokoa. Ni jaribio la kukata tamaa la kuleta makundi yenye kutofautiana kwenye jukwaa moja na limeathirika tangu mwanzo," msemaji wa taifa wa BJP Tom Vadakkan aliiambia DW. "Hautafanikiwa. Muundo wake una dosari," aliongeza.

Vita vya 'INDIA dhidi ya NDA vyazidi kuchangamsha'

BJP wiki iliyopita pia ilisherehekea miaka tisa madarakani na kuandaa mkusanyiko wa chama tawala cha National Democratic Alliance (NDA) kinachoongozwa na chama tawala, cha kwanza baada ya miaka, kuadhimisha miaka 25 ya muungano huo.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiwahutubia wabunge wa Bunge la IndiaPicha: AP Photo/picture alliance

NDA inajumuisha vyama 38, vingi vikiwa ni vikundi vidogo vyenye uwepo mdogo katika sehemu za nchi. Imepungua kama muungano tangu Modi aingie madarakani mnamo 2014 na kuchaguliwa tena mnamo 2019 huku akikiongoza chama cha BJP kwa ushindi mkubwa, na kupunguza ushawishi wa washirika wa muungano.

Soma pia:Upinzani wasusia uzinduzi wa jengo jipya la bunge uliofanywa na Mordi

Lakini BJP inaufufua muungano wa NDA sasa kwani haitaki kuacha chochote kwa nafasi ili kushinda muhula wa tatu, Neerja Chowdhury, mchambuzi wa kisiasa ambaye ameshughulikia chaguzi 10 zilizopita nchini India, aliiambia DW.

"Vita vya INDIA dhidi ya NDA vimekuwa vya kusisimua ghafla kwa sababu BJP inafanya kila kitu kupata mafanikio na upinzani unapambana. Maoni ya viongozi wa upinzani kwenye jukwaa moja yametoa msukumo wa kisaikolojia kwa kambi inayopinga BJP," alisema.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW