1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndia

India na Pakistan zaanza mikakati ya kuwahamisha watu

12 Juni 2023

India na Pakistan zimeanza mikakati ya kuwahamisha watu wapatao 80,000 kufuatia hatari ya kimbunga kinachotarajiwa kupiga maeneo ya pwani baadaye wiki hii.

Guam | Taifun Mawar
Picha: Adam Brown/U.S. Coast Guard/AP/picture alliance

Kulingana na Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Pakistan, kimbunga hicho kilichopewa jina la Biparjoy kitatokea kaskazini mwa Bahari ya Hindi na kuelekea kusini mwa Pakistan katika mkoa wa Sindh na ukanda wa pwani wa jimbo la magharibi la India la Gujarat.

Kimbunga chatarajia siku ya Alhamisi

Kimbunga hicho kinatarajiwa kuyapiga maeneo hayo siku ya Alhamisi na kitakuwa na kasi hadi kufikia kilometa 200 kwa saa. Mwaka 2021, kimbunga Tauktae kiligharimu maisha ya watu 174 na kusababisha uharibifu wa zaidi ya dola bilioni 1.57.