India na Pakistan zabadilishana orodha ya maeneo ya kinuklia.
2 Januari 2008Matangazo
New Delhi. India na Pakistan zimebadilishana orodha ya maeneo yake ya kinuklia na vifaa. Orodha hiyo ilikabidhiwa kwa wakati mmoja na nchi hizo chini ya makubaliano ya muda wa miaka 17 yaliyofikiwa hapo Desemba 31, 1988. Chini ya makubaliano hayo nchi zote zinatakiwa kutoshambulia maeneo ya nchi nyingine ya kinuklia. Nchi hizo jirani zenye silaha za kinuklia zimerejea katika majadiliano ya amani mwaka 2004.