1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

India: Rahul Gandhi apoteza kiti chake cha Bunge

25 Julai 2023

Chama cha upinzani cha Congress nchini India kimepata pigo baada ya bunge kuamua kumfukuza kiongozi wake, Rahul Gandhi kwa kutoa matamshi ambayo jamii nchini humo imeyachukulia kama ni kumtusi Waziri Mkuu Narendra Modi.

Der Generalsekretär der indischen Kongresspartei Rahul Gandhi
Picha: UNI

Hatua hiyo imechukuliwa siku moja baada ya mahakama kumtia hatiani mwanasiasa huyo wa upinzani Rahul Gandhi kutokana na kutoa matamshi yaliyopokelewa kama ni kumtusi Waziri Mkuu Narendra Modi.

Mwanasiasa Rahul Gandhi kiongozi wa chama cha upinzani cha Congress, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili lakini akaachiliwa kwa dhamana huku mawakili wake wakisema watakata rufaa kupinga hukumu ya siku ya Alhamisi iliyotolewa dhidi ya mteja wao. Hata hivyo, hukumu hiyo imemfanya mwanasiasa huyo Gandhi kuwa hastahili kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge kwa mujibu wa notisi kutoka kwa katibu wa bunge.

Katikati mwenye fulana nyeupe kiongozi wa chama cha upinzani nchini India Rahul Gandhi alipowasili mahakamani katika mji wa Surat, India tarehe 23.03.2023.Picha: AP/picture alliance

Gandhi alitoa maneno hayo wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita ambao  chama tawala cha Hindu-nationalist Bharatiya Janata Party (BJP) cha Waziri Mkuu Narendra Modi kiliibuka mshindi. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanachama wa chama tawala cha Modi anayeitwa Purnesh Modi, ambaye alizingatia maoni ambayo Gandhi aliyatoa kwenye hotuba yake yam waka 2019 alipowataja wafanyabiashara wawili waliotoroka nchini, ambao wote wawili wana majina ya Modi. Na hapo Gandhi alisikika akiuliza "Inakuwaje wezi wote wana majina ya Modi?"

Soma:Kiongozi wa upinzani ahukumiwa kifungo cha miaka 2 India

Hakimu aliyetoa hukumu alisema kifungo cha miaka miwili jela kilikuwa halali kwa sababu kutoa hukumu nyepesi kwa mtuhumiwa kungetoa ujumbe usio sawa kwa watu". Kiongozi wa chama cha Upinzani cha Congress cha nchini India  Mallikarjun Kharge amesema

Gandhi, mwenye umri wa miaka 52, ndiye kiongozi mkuu wa chama cha Congress, kilichowahi kuwa na nguvu kubwa ya siasa nchini India, na kinachojivunia juu ya kuukomesha utawala wa mkoloni Uingereza, lakini sasa kimebaki kuwa kivuli cha uwezo wake wa zamani.  Rahul Gadhi ni mzaliwa katika nasaba maarufu ya kisiasa ya India ni mwana, ni mjukuu na kitukuu cha mawaziri wakuu wa zamani, kuanzia kiongozi wa uhuru wa India Jawaharlal Nehru.

Katika siasa za sasa za nchini India anajitahidi lakini si rahisi kuushinda ushawishi mkubwa wa Narendra Modi kwa wapiga kura Wahindu walio wengi nchini India.

Waziri Mkuu wa India Narendra ModiPicha: Sergei Bobylev/Sputnik/Kremlin Pool Photo/AP/picture alliance

Hukumu hiyo iliyotolewa jana Alhamisi ni baada ya miezi miwili tangu Rahul Gandhi alipohitimisha matembezi ya kuzunguka nchini kote ya kilomita 4,000 kutoka kwenye ncha ya kusini ya India hadi katika jimbo la Kashmir kwenye milima ya Himalaya katika jitihada za kukifufua chama chake na kujenga sura mpya katika kile alichokiita Bharat Jodo Yatra, kwa maana Tuungane katika mwendo wa kuisogeza mbele India.

Vyanzo: AFP/RTRE

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW