1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

India, Urusi zakubaliana kutanua ushirikiano wa kibiashara

5 Desemba 2025

India na Urusi zimekubaliana kuhusu mpango wa ushirikiano wa kiuchumi utakaotanua biashara yao hadi mwaka wa 2030. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Indien Neu-Delhi 2025 | Handschlag zwischen Wladimir Putin und Narendra Modi beim Treffen im Hyderabad House
India na Urusi zimekubaliana kuhusu mpango wa ushirikiano wa kiuchumi utakaotanua biashara yao hadi mwaka wa 2030Picha: Adnan Abidi/REUTERS

Modi ameitaja ziara ya Putin kuwa kubwa na yenye kubeba umuhimu wa kihistoria kwa kuzingatia kwamba Putin aliitembelea India mara ya mwisho mwaka 2021. Putin ambaye yuko ziarani Urusiamesema ataendelea na "usafirishaji usiokatizwa" wa mafuta kwenda India, huku New Delhi ikikabiliwa na shinikizo kubwa la Marekani la kuacha kununua mafuta kutoka Moscow.

Putin amemwambia Modi kuwa Urusi ni muuzaji wa kuaminika wa mafuta, gesi, makaa ya mawe, na kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo ya nishati nchini India.

Ushirikiano huu wa India na Urusi unaonesha ni kwa jinsi gani sasa NewDelhi italazimika kuweka urari katika mahusiano yake baina ya Moscow na  Marekani hasa kwa kuzingatia kwamba Marekani nimekuwa ikiishinikiza India kuutathmini upya uhusiano wake na Moscow.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW