India yamfukuza balozi wa Canada
19 Septemba 2023Uamuzi wa New Delhi umefanyika siku moja tu baada ya Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, kusema kuwa kulikuwa na madai ya kuaminika kwamba India ilikuwa inahusika na mauaji ya mwanaharakati Hardeep Singh Nijjar aliyeuawa Juni 18 nje ya kituo cha Utamaduni wa Singasinga kilichoko Surrey, British Columbia.
Soma zaidi: OTAWA-Masingasinga wawili waachiwa huru kutokana na kesi ya uripuaji wa ndege ya abiria ya India mwaka 1985
India imekanusha madai hayo, ikisema ni ya kipuuzi.
Canada nayo imemfukuza mwanadiplomasia wa India, huku mzozo wa mauaji hayo ukiongezeka.
Nijjar alikuwa akiandaa kura ya maoni isiyo rasmi kuhusu uhuru wa jamii ya Singasinga kutoka India.
Mwanaharakati huyo alikuwa akitafutwa na maafisa wa India kwa madai ya kuhusika katika shambulizi linalodaiwa kumlenga kiongozi wa madhehebu ya Kihindu nchini India.