Janga
India:Tumekamilisha oparesheni ya uokoaji mkasa wa treni
4 Juni 2023Matangazo
Katibu kiongozi wa jimbo la mashariki la Odisha Pradeep Jena, amesema idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo iliyotokea Ijumaa imerekebishwa kutoka 288, baada ya kubainika kuwa baadhi ya maiti zilikuwa zimehisabiwa mara mbili.
Amewaambia waandishi wa habari kuwaidadi hiyo haina uwezekano wa kuongezeka baada ya kukamilika kwa operesheni hiyo.
Karibu watu 1,200 walijeruhiwa wakati treni ya abiria ilipogonga nyingine ya mizigo iliyokuwa imesimama, kuacha njia na kugonga treni nyingine ya abiria iliyokuwa inapita katika upande mwingine karibu na wilaya ya Balasore.
Soma pia:Hakuna manusura wengine wa ajali ya treni India
Zaidi ya watu 900 wameruhusiwa kutoka hospitali wakati 260 walikuwa wanaendelea kutibiwa, huku mgonjwa mmoja akiwa hali mahututi.