INDONESIA NA MSIBA WA MAFURIKO
4 Januari 2005Indonesia imekumbwa na mmoja kati ya misiba mikubwa kabisa katika historia ya nchi hii.Idadi rasmi kuhusu watu wake waliofariki,majeruhi na waliopoteza maskani,serikali ya indonesia mjini Jakarta, haitaki tena kutangaza .kwani wiki baada ya msiba wa mafuriko ya zilzala iliopiga Sumatra,baadhi ya maeneo ya msiba yanaweza kufikiwa tu kwa njia ya anga.
Waindonesia waliovuka na maisha yao,wanakufa na njaa,watu wanahofia kuambukizwa na magonjwa na shehena za misaada haziwafiki wote waliokumbwa na maafa haya.
Miezi michache tu baada ya kushika madaraka kama rais mpya wa Indonesia,Susilo Bambang Yudhoyono amekabiliwa na mtihani mkubwa:Kuliko nchi nyengine yoyote,Indonesia ndio ilioathirika mno na zilzala na mafuriko.kinachopiga msumari juu ya donda ni kuona msiba huu umepiga eneo ambalo tayari limeathrika na vita vya kienyeji vya mungo mzima na kutokana na sheria ya vita iliotangazwa tangu mwaka 2003,halikua na taasisi za kiraia zilizoweza kufanya kazi.Kwamba wiki chache kabla msiba huu kutokea, Gavana wa eneo hili alitiwa korokoroni kwa mashtaka ya rushua, ni kizingiti kingine kinachoukumba mkoa huu na mengine ya Indonesia.
Hali ya kisiasa ya INDONESIA INATATIZA JUHUDI ZA MASHIRIKA YA MISAADA YA KIMATAIFA:
Katika sehemu kubwa ya nchi zilizokumbwa na balaa la TSUNAMI,kumekuwapo matawi ya nchini ambayo yameweza kushirikiana na yale ya kimataifa ili kutayarisha mipango ya kueneza misaada kwa wahanga.
Katika eneo la ACEH hali ni tofauti:Chombo pekee pekee kinachotoa misaada kwa wingi na chenye zana za kusambaza misaada ni Jeshi la Indonesia.
Tangu 1976 vita vya kienyevi vimepamba moto huko Aceh kati ya Jeshi la serikali ya Indonesia na Jeshi la Ukombozi linalogom,bea uhuru kwa mkoa wa Aceh kutoka Indonesia.Kiasi cha watu 12.000 wameuwawa katika vita hivyo.
Kwa hali ilivyo, huu ni mzigo mzito kwa rais mpya wa Indonesia.Tangu kushika madaraka, rais Bambang Yudhoyono amekuwa akisisitiza kwamba akisaka suluhihso la amani kwa mzozo wa Ache na wa maeneo mengine ya Indonesia.Hivyo hasaki suluhisho kwa njia ya mtutu wa bunduki sawa na vile rais aliemtangulia alivyojaribu.
Na kama vile baadhi ya taarifa kutoka eneo hili la msukosuko zinavyobainisha hujuma za kijeshi zinasonga mbele licha ya ahadi aliotoa rais Yudhoyono baada ya balaa la TSUNAMI.
Baada ya miaka 30 ya utawala wa kidikteta, Jeshi nchini Indonesia limesalia kuwa turufu kubwa ya kisiasa.Kwa jicho hili basi, rais Yudhoyono amecheza uzuri karata zake.Ameifuta sheria ya hali ya vita, akafungua mipaka ya kuingilia Aceh na kuyapa mashirika ya kimataifa fursa za kuingia bila pingamizi mkoani Aceh.
Kwa njia hii ugomvi wa kisiasa huko Aceh umefaidika kupata kile ambacho kwa miaka mingi kimekosekana:ulimwengu kujua kinapita nini huko.Hali hii ya uwazi itawafanya tangu waasi wa ACEH hata majeshi ya serikali kujizuwia kufanya madhambi na rais Yudhoyono amedhibiti upya turufu ya kisiasa.
Hali ikoje kuhusu uongozi wa kukabiliana na msiba uliozuka huko ?
Kwa jicho la maafa makubwa yaliosababishwa na zilzala na mafuriko huko Aceh,athari za kuhilikisha umma mzima zimedhibitiwa kwa muda mfupi.Hata ikiwa awali kamera nyingi zilielekezwa katika maafa yaliopiga pwani za watalii wa kimagharibi kisiwani sri Lanka na Thailand, mkoani Aceh,jamii ya kimataifa na mashirika ya misaada ya Indonesia haraka yametenda kinachowezekana kuwaopunguzia shida walionusurika na maisha.
Msiba wa mafuriko haya umebainisha jambo moja wazi:Kuna mpaka wa kile mwanadamu awezacho kufanya.Nchini Indonesia hata pangekuwapo chombo cha kuonya na mapema juu ya balaa hili,isingesaidia kitu.Kwani, baada ya zilzala,mafuriko yalifuata tena mnamo muda wa dakika chache pamoja na athari zake kubwa za kuhilikisha umma.hakuna mpango wowote wa kukabiliana na maafa ungeliweza kuzuwia balaa hilo.
Sasa Aceh inakabili miaka mingi ya kujenga upya:Inabidi ACEH kutambua kilio chake cha muongo mmoja cha uhuru na kujitenga kutoka sehemu iliobaki ya Indonesia,hakitaisaidia kitu.Kwani pekee yake Aceh haiwezi kudumu na haifui dafu.