1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Indonesia yasimamisha uokoaji baada ya volkano kuripuka tena

4 Desemba 2023

Maafisa wa idara ya uokoaji nchini Indonesia wamelisimamisha zoezi la kuwatafuta wapanda milima stadi 12 baada ya volkano kwenye Mlima wa Marapi kuripuka tena na kutoa majivu ya moto yaliyofikia umbali wa mita 800.

Volkano ya Mlima Marapi ikiripuka.
Volkano ya Mlima Marapi ikiripuka.Picha: Ardhy Fernando/AP/picture alliance

Hapo awali miili ya wapanda mlima 11 ilipatikana wakati wa kuwatafuta waliopotea lakini juhudi za kuwaondoa zilishindikana kutokana na kuripuka tena kwa mlima huo.

Mkuu wa Idara ya Ukoaji, Abdul Malik, alisema zoezi hilo lingeendelea hali itakapotengemaa.

Mlima wa Marapi uliripuka siku ya Jumapili (Disemba 3) na kutoa majivu ya moto.

Soma zaidi: Vifo Indonesia kufuatia mripuko wa volkano sasa ni 34

Mlima huo umewekwa katika kiwango cha juu cha tahadhari tangu mwaka 2011 na hivyo kuwapiga marufuku wanaofanya shughuli za kuupanda.

Wapanda milima stadi 75 walianza kuupanda mlima huo siku ya Jumamosi na kufikia juu karibu mita 2,900 ambako walikwama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW