1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Indonesia yaweza kutuma vikosi vyake Gaza iwapo itahitajika

1 Juni 2024

Rais Mteule wa Indonesia Prabowo Subianto amesema kwamba nchi yake iko tayari kutuma wanajeshi wa kulinda amani ili kusaidia kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza.

Singapore | Mkutano wa usalama wa Shangri-La
Rais Mteule wa Indonesia Prabowo SubiantoPicha: Nhac Nguyen/AFP/Getty Images

Akizungumza katika Mkutano wa masuala ya usalama wa Shangri-La unaofanyika mjini Singapore, Prabowo amesema pendekezo la kusitisha mapigano la awamu tatu lililotolewa na Rais wa Marekani Joe Biden ni hatua iliyopigwa katika muelekeo unaostahili. 

"Ingawa inabidi tuangalie na kuchunguza kwa makini kilichopo ndani ya pendekezo hili lililotangazawa na rais Joe biden, lakini tunaliona kama hatua muhimu inayokwenda katika muelekeo unaohitajika, tunaliona kama hatua muhimu iliyochukuliwa katika kusonga mbele," alisema Prabowo Subianto.

Wizara ya afya ya Gaza yasema karibu watu 36,000 wameuawa Gaza

Rais huyo Mteule wa Indonesia aliye na miaka 72, amesema iwapo wataombwa na Umoja wa Mataifa kuchangia katika hatua za kusitisha mapigano basi wako tayari kutuma kikosi cha kulinda amani kufuatilia makubaliano ya kusitisha mapigano pamoja na kutoa ulinzi na usalama kwa pande zote zinazohasimiana. 

Subianto ambaye ni jenerali wa zamani wa vikosi maalum na Waziri wa sasa wa ulinzi wa Indonesia, atachukua urais wa taifa hilo lenye idadi kubwa ya waislamu mwezi Oktoba mwaka huu. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW