1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Infantino: Kombe la dunia la Qatar 2022 litakuwa kivutio

11 Februari 2022

Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA Gianni Infantino amesema leo kuwa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia nchini Qatar yatakuwa mfano mzuri wa kuandaa matukio ya michezo katika siku za usoni

 FIFA World Cup Fußball Weltmeisterschaft 2022 Logo Symbolbild
Picha: Aleksandr Gusev/Zumapress/picture alliance

Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA Gianni Infantino amesema leo kuwa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia nchini Qatar yatakuwa mfano mzuri wa kuandaa matukio ya michezo katika siku za usoni wakati kukiwa na mzozo wa kiafya. FIFA ilitangaza wiki hii kuwa maombi yametolewa kwa ajili ya tiketi milioni 17 za kuhudhuria Kombe la Dunia la kwanza kufanyika Uarabuni na ikawahakikishia mashabiki kuhusu hatua za usalama wakati wa mkutano wa afya wa mtandaoni ulioandaliwa na mamlaka za Qatar. Infantino amesema kandanda lina wajibu wa kuhakikisha kuwa hili sio tu Kombe la Dunia bora zaidi kuwahi kuandaliwa bali pia litafanyika katika mazingira bora zaidi ya kiafya. Kombe la Dunia la Qatar litaanza Novemba 21 hadi Desemba 18 mwaka huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW