1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ingabire: Matumaini ya uhuru wa vyama vya kisiasa Rwanda  

Oumilkheir Hamidou
17 Septemba 2018

Baada ya kuachiwa huru, kiongozi wa chama cha upinzani cha FDU-Inkinge, nchini Rwanda bibi Ingabire Umuhoza Victoire aelezea matumaini ya kuiona Rwanda ikifungua milango kwa vyama vyengine vya kisiasa. 

ARCHIV Oppositionsführerin Victoire Ingabire in Ruanda festgenommen
Picha: picture alliance/dpa/O. Boulot

Kiongozi wa chama cha upinzani cha FDU-Inkinge, nchini Rwanda bibi Ingabire Umuhoza Victoire ameachiwa huru mwishoni mwa wiki kutokana na amri ya rais Paul Kagame. Katika mahojiano na DW bibi Ingabire Victoire ameelezea matumaini ya kuiona Rwanda ikifungua milango kwa vyama vyengine vya kisiasa. 

Katika mahojiano hayo  na DW mwenyekiti wa chama cha Front Democratic Un ifié-FDU Inkinge, Ingabire Umuhoza Victoire amezungumzia jinsi alivyostaajabishwa na uamuzi wa kumuachia huru na kusema: "Bila ya shaka nilishangaa kwa sababu nilipata habari usiku na sikuweza kulala kwasababu sikuelewa kama ningeachiwa huru haraka."

Bibi Ingabire alikuwa atumikie kifungo cha miaka 15 jela. Akielezea jinsi hali ilivyokuwa jela kiongozi huyo wa chama cha FDU  anazungumzia shida alizokutana nazo miaka mitano ya mwanzo ambayoanasrema ilikuwa migumu kwangu kwasaabu alikuwa amefungwa peke yake na hakuwa na mtu yeyote wakuzungumza nae.Na miaka mitatu ya mwisho lakini alitumikia kifungo pamoja na wafungwa wengine kwa hivyo angalao alikuwa na watu wakuzungumza nao.

Ingabire anahisi milango ya kisiasa imeanza kufunguka hivi sasa nchini RwandaPicha: Reuters/J. Bizimana

Milango ya kisiasa imeanza kufunguka Rwanda?

Katika mahojiano yake na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa huru Jumamosi iliyopita, bibi Ingabire alisema anahisi milango ya kisiasa imeanza kufunguka hivi sasa nchini Rwanda. Hoja hiyo ameitoa alipohojiwa na DW aliposema: 

"Nimesema hivyo kwasababu nimeona wiki zilizopita chama cha Green kwa mfan o kiliruhusiwa bungeni na wiki mbili baadae nikaachiwa huru. Na mnatambua akwamba serikali imeniachia huru katika wakati ambapo chama achangu cha kisiasa kimetangaza nimechaguliwa tena kukiongoza chama hicho. Kwa hivyo serikali inatambua kwamba mie ndie kiongozi wa chama katika upande wa upinzani. Ikiwa wamekubali kuniachia huru,nahisi wanajaribu kufungua miango ya kisiasa nchini Rwanda. Na nnataraji watafanya mengi zaidi kwasababu kuna viongozi wengine wa vyama vya kisiasa walioko jela kama mnavyojua."

Amewataja akina bibi Diane Rwigara ambae bado yuko jela, Mushaidi Deo na kusema anataraji wote hao wataachiwa huru haraka.

Mwenyekiti wa chama cha FDU amezungumzia pia umuhimu kwa serikali kudhamini usalama wao.

Mwanfdishi: Hamidou Oummilkheir/DW

Mhariri: Mohammed Khelef