1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Inspekta wa polisi auawa Nigeria

20 Septemba 2021

Watu wenye silaha wamemuua inspekta wa polisi kusini mashariki mwa Nigeria.

Nigeria Abuja | Sicherheitspersonal | Entführte Studenten
Picha: Nasu Bori/AFP/Getty Images

Msemaji wa polisi katika jimbo la Anambra, Ikenga Tochukwu amesema shambulizi hilo limetokea jana baada ya watu wenye silaha walivamia gari la polisi lililokuwa likifanya doria kwenye mji wa kibiashara wa Onitsha katika jimbo hilo.

Tochukwu amesema washambuliaji hao walitumia gari aina ya Sienna na walianza kulifyatulia risasi gari la polisi kwenye eneo la makutano la Ukegbu.

Ameongeza kusema kuwa baada ya majibizano ya risasi kwa bahati mbaya inspekta mmoja wa polisi aliuawa. Maafisa wengine wa polisi walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na mashambulizi ya hivi karibuni, lakini polisi mara nyingi huwa inalishutumu kundi linalopigania uhuru wa watu wa asili ya Biafra, IPOB ambalo linadai serikali huru ya watu wa kabila la Igbo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW