1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

INSTANBUL:Kamera zanasa picha ya muuaji wa kujitolea muhanga maisha

17 Novemba 2003
Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki amesema katika mahojiano yaliyochapishwa leo hii kwamba kamera za usalama zimeweza kuchukuwa picha ya mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha aliyeliendesha gari lililosheheni mabomu katika mojawapo ya sinagogi mahala pa kuendesha ibada za Mayahudi mjini Instanbul mwishoni mwa juma. Abdulkadir Aksu pia ameahidi kwamba Uturuki itawatafuta wale waliohusika na miripuko hiyo iliyoharibu vibaya masinagogi mawili ambapo waumini wa Kiyahudi walikuwa katika ibada hapo Jumamosi na kuuwa watu 27 na kujeruhi wengine zaidi ya 300. Ameliambia gazeti la Vatan kwamba mashambulizi hayo yamefanywa na washambuliaji wawili wa kujitolea muhanga maisha ambao waliripuwa mabomu yaliokuwa na nguvu kubwa yaliokuwemo ndani ya magari wakati magari hayo yakipita kwenye masinagogi ya Neve Shalom na Beth Israel katikati ya mji wa Instanbul.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW