1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaUkraine

Intaneti yarejea Kyiv baada ya shambulizi la mtandao

15 Desemba 2023

Siku chache baada ya shambulio kubwa la mtandaoni, moja ya kampuni kubwa za simu nchini Ukraine imerejesha huduma za intaneti kote nchini.

Cyberangriffe: Ermittler zerschlagen großes Hacker-Netzwerk Hive ransomware
Picha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Kampuni ya Kyivstar inayotoa huduma za intaneti imeeleza kuwa, mtandao wa intaneti sasa unapatikana tena katika mji mkuu Kiev, kama ilivyothibitishwa pia na mwandishi wa shirika la habari la dpa.

Huduma za intaneti pia zinapatikana katika eneo la magharibi mwa nchi, ambalo kwa kiasi kikubwa halijaathirika na vita dhidi ya Urusi.

Watumiaji wa mitandao wamefanikiwa kutumia intaneti na kufanya mawasiliano kwa njia ya simu tangu jana Alhamisi. Huduma za mtandao za kampuni ya Kyivstar zilikatika kabisa mnamo siku ya Jumanne, katika tukio ambalo linadaiwa kuwa ni hujuma iliyofanywa na Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW