1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Inter Milan yatinga fainali ya Champions League

7 Mei 2025

Klabu ya soka ya Inter Milan imejikatia tiketi ya kucheza fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, Champions League.

Champions League 2025 | Nusu fainali | Inter Milan vs. FC Barcelona
Mchezo kati ya Inter Milan na Barcelona ulipigwa kwenye dimba la San Siro.Picha: Carabelli/Beautiful Sports/IMAGO

Hiyo ni baada ya kupapatua ushindi mbele ya vigogo Barcelona katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ulipigwa usiku wa kuamkia leo.

Mtanange huo kwenye dimba la San Sirro mjini Milan ulikwenda hadi dakika za nyongeza, na Inter ikamudu kuibamiza Barcelona bao 4-3. 

Matokeo hayo pamoja na yale ya mechi ya mkondo wa kwanza ambayo timu hizo zilitoka sare ya bao 3-3, yalimaanisha Inter ilikuwa imefunga mabao 7 dhidi ya 6 ya Barcelona. 

Ushindi huo unaiwezesha Inter Milan kucheza fainali yake ya pili ya Champions League ndani ya kipindi cha misimu mitatu.

Vijana hao wa kocha Simone Inzaghi watasubiri matokeo ya mechi ya leo ya nusu fainali mkondo wa pili kati ya Arsenal na  Paris St. Germain kujua timu watakayokutana nayo fainali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW